Home » Kanisa La Methodist Lawarudisha Washirika Waliotimuliwa

Kanisa La Methodist Lawarudisha Washirika Waliotimuliwa

Kanisa la Methodist nchini Kenya limewarudisha waumini wao waliotengwa kuendelea kuabudu pamoja nao baada ya mahakama kukubali kurejesha haki zao kufuatia mizozo ya uongozi ambayo imekuwa ikiendelea tangu mwaka 2021.

 

Kaimu Askofu Mfawidhi Mchungaji Isaya Deye Alhamis akitoa taarifa kwa umma aliishukuru Mahakama kwa kukubaliana na uamuzi uliotolewa na Kamati ya Kudumu ya Mkutano huo wa kurejesha haki na marupurupu ya watumishi na wanachama.

 

Kwa mujibu wa Askofu Deye, uamuzi wa mahakama uliotolewa Juni 12, 2023, ulimzuia aliyekuwa msimamizi wa kanisa hilo Joseph Ntombura kufanya kazi yoyote akidai kuwa askofu msimamizi wa kanisa la Methodist.

 

Korti pia iliamuru kuondolewa kwa wanachama walioachishwa kazi ambao majina yao yalichapishwa katika gazeti la kila siku la 2021.

 

Haya yalianza kutekelezwa baada ya kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi ya aliyekuwa askofu msimamizi kukaa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

 

Kanisa sasa linawakaribisha washiriki wowote ambao huenda waliondoka kwa sababu ya kutoridhishwa na uongozi wa Kanisa wakati huo, likiwahakikishia washiriki wake, washirika na serikali kutatua kwa amani masuala yote yaliyotokea hapo awali.

 

Wakati uo huo, kanisa linamwomba Askofu wa zamani Ntombura kufuta mawasiliano yote ambayo amekuwa akituma kwa mashirika na watu mbalimbali wanaodai kuwa askofu msimamizi wa kanisa la Methodist nchini Kenya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!