Home » Ruto Apeleka Ajenda Ya Bottom-up Uswizi

Rais William Ruto hii leo Alhamisi amesistiza kwamba utawala wake una nia ya kubadilisha kikamilifu uchumi wa nchi, kupitia miradi mbalimbali.

 

Akiongea wakati wa Kongamano la Kimataifa la Wafanyakazi huko Geneva, Uswizi, Ruto alisema serikali yake imejitolea kutekeleza ajenda ya mabadiliko ya kiuchumi kutoka chini kwenda juu.

 

Zaidi ya hayo, Mkuu wa Nchi alisema Kenya imeingia katika ushirikiano wa kuendeleza miundombinu muhimu ili kutoa maeneo 25,000 ya Wi-Fi katika vituo vya soko kote nchini.

 

Kuhusu ajira, Rais alisema utawala wake utawawezesha mamilioni ya vijana kuchangamkia fursa zinazojitokeza za mfumo ikolojia wa kazi za kidijitali.

 

Hii, kulingana na Ruto itaweza kuwaunganisha na kuwashirikisha Wakenya duniani kote kutoka kwa urahisi wa vijiji vyao.

 

Kuhusu masuala ya biashara, Rais alisema Afrika inachangia asilimia 3 pekee ya biashara ya kimataifa, ingawa ni nyumbani kwa asilimia 17 ya watu wote duniani.

 

“Biashara ya ndani ya Afrika kwa sasa inafikia asilimia 15 tu. Wasifu wa kibiashara wa bara letu unaonyesha kuwa hatujaanza kufanya kazi kwa kiwango kinacholingana na uwezo wetu, na hii inadhoofisha uwezo wetu wa kutimiza Ajenda 2063 na malengo ya maendeleo endelevu,” alisema. .

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!