Home » Migori :Muungano Wa Wafanyikazi Wapinga Mswada Wa Fedha

Migori :Muungano Wa Wafanyikazi Wapinga Mswada Wa Fedha

Ofisi ya Gavana Migori /Picha kwa hisani

Katibu Mtendaji wa chama cha wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Migori Silavnace Araja amewataka wajumbe wa bunge la kitaifa kukataa Mswada wa Fedha wa 2023 akisema kuwa mapendekezo katika mswada huo yataathiri wafanyikazi wa umma.

Araja amesema huu ni wakati wa wajumbe wa Bunge hilo kusimama kidete na wapiga kura na kutetea maslahi yao bungeni.

 

Amesema wapiga kura wanatazama kwa makini wabunge wakisema kwamba wale wanaounga mkono mswada huo watakutana nao kwenye uchaguzi ujao wa 2027.

 

Katibu mtendaji wa chama cha wafanyikazi wa Serikali ya Kaunti ya Migori amesema wafanyikazi hao wanapinga mapendekezo ya kukatwa kwa mishahara ya asilimia 3 kwa ushuru wa Nyumba akisema kuwa wafanyikazi kadhaa tayari wamejenga nyumba zao na wengine pia wamejipanga.

 

Kulingana na Araja wafanyakazi hao hawapendezwi na nyumba za bei nafuu ambazo serikali inapanga kujenga.

 

Aidha Amesema wanaopenda nyumba za bei nafuu wachangie lakini wasiopenda lazima wasamehewe katika mpango huo.

 

Kadhalika Katibu huyo mkuu amesema atawahimiza wafanyikazi kupinga Mswada wa Fedha wa 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!