Home » Viongozi Wasusia Sherehe Za Madaraka Nyeri Na Migori
Migori Nyeri Skip Madaraka Celebrations

Sherehe ya Madaraka Picha kwa hisani

Makamishna wa Kaunti ya Migori na Nyeri wameongoza halfa la Madaraka Day katika nyadhifa zao mbalimbali huku wakiwakashifu viongozi wao wa kisiasa waliowachagua kwa kukosa kuhudhuria sherehe za Madaraka zilizoadhimishwa Alhamisi.

 

Makamishna wa Kaunti waliongoza sherehe hizo ambazo ziliadhimishwa kibinafsi katika kaunti zote.

 

Kamishna wa Kaunti ya Nyeri Pius Murugu alisema kukosekana kwa viongozi wa kisiasa kunafanya kuwa vigumu kwa wasimamizi kushughulikia baadhi ya masuala yanayoathiri wenyeji.

 

Naye Kamishna wa Kaunti ya Migori David Gitonga kwa upande wake pia alikashifu kutohudhuria kwa viongozi wa kisiasa akibainisha kuwa hakuna kiongozi hata mmoja aliyechaguliwa alifika kwa hafla hiyo wakiwemo wawakilishi wadi.

 

Aidha Alisisitiza umuhimu wa mkusanyiko huo akisema sherehe za kitaifa si za serikali iliyoko madarakani bali ni za watu wa Kenya, na hivyo basi kuwataka viongozi waliochaguliwa na wananchi kukumbatia sherehe hizo.

 

Hotuba ya Gavana wa Migori Ochilo Ayacko ilisomwa na msimamizi wa kaunti ndogo ya Suna Mashariki Dustan Chacha wakati wa sherehe hizo.

 

Baadhi ya wananchi waliozungumza na wanahabari walisema kuna haja ya viongozi waliochaguliwa na wananchi kukumbatia sherehe za kitaifa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!