Home » Rais Ruto: Ninaahidi Kufanya Kazi Na Viongozi Wote

Rais William Ruto amewahakikishia wakenya kuwa atashirikiana na viongozi wote kwa ajili ya ustawi wa Kenya.

 

Akizungumza huko Embu wakati wa sherehe za Madaraka Day , Ruto amesema kuwa Wakenya wanastahili viongozi wanaoweka kando tofauti za kisiasa na kufanya kazi ili kutoa huduma ipasavyo.

 

” Nawahakikishia kwanza nitafanya kazi na hawa viongozi wote, kupeleka Kenya mbele.

 

Hii ina maana: Ninataka kuwahakikishia kwamba nitafanya kazi na viongozi wote ili kuwasogeza Wakenya mbele.

 

Mwezi uliopita akiwa Isiolo, Rais William Ruto alisema kuwa wakati umewadia kwa serikali kukaribiana na upinzani.

 

Alisisitiza kuwa Kenya ni moja na inafaa kuwa na serikali moja pekee ya kuwafikishia raia wake.

 

“Ni wakati wa sisi kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya nchi yetu,” Ruto alisema.

 

“Hakuna nchi ya serikali pekee na nyingine ya upinzani. Serikali ninayoongoza ni ya Wakenya wote,” aliongeza.

 

Hata hivyo, viongozi wakuu wa upinzani akiwemo mkuu wa Azimio Raila Odinga wamekosa sherehe za kitaifa za Madaraka Day mwaka huu katika uwanja wa Moi Embu.

 

Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa upinzani kuruka tukio muhimu kama hilo.

 

Wakati wa sherehe ya kwanza ya siku ya kitaifa ya Ruto Oktoba 20, 2022 kuadhimisha Siku ya Mashujaa, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ndiye kiongozi pekee wa upinzani aliyehudhuria sherehe hizo zilizofanyika Uhuru Gardens, Nairobi.

 

Siku chache kabla ya sherehe hizo, Raila alikuwa ameondoka nchini Oktoba 16, 2022 na kuelekea India.

 

Raila pia aliruka sherehe ya Jamhuri Day mnamo Desemba 12, 2022, baada ya kuondoka nchini kuelekea Marekani.

 

Hii ni mara ya tatu kwa Ruto kuwa anaongoza nchi kuadhimisha Sikukuu ya Kitaifa tangu aingie madarakani Septemba 13, 2022.
Rais ametumia fursa hiyo kuzindua Hustler FUND awamu ya pili

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!