Home » Rais Wa Comoros Amshukuru Ruto

Rais wa Comoro Azali Assoumani amemshukuru Rais William Ruto kwa kumuunga mkono kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Assoumani alichukua nafasi ya mwenyekiti wa AU mwezi Februari mwaka wa 2023.

 

”Ninashukuru Kenya kwa kuunga mkono mgombeaji wa Comoro kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa 2023,” alisema.

 

Akihutubia taifa wakati wa sherehe za Siku ya Madaraka katika uwanja wa Moi, Embu, Assoumani alipongeza maendeleo ya Kenya tangu uhuru.

 

”Kenya imepata maendeleo makubwa tangu uhuru, natoa heshima kwa baba wa uhuru wa Afrika,” alisema.

 

 

Kiongozi huyo wa Comoro alisema kuwa wakati baadhi ya Nchi za Kiafrika zikipunguza kasi ya kupigania uhuru baada ya uhuru, Kenya iliharakisha maendeleo yake.

 

”Nina furaha sana kwamba mliharakisha uhuru wenu kama nchi na miaka 60 baadaye Kenya inaheshimiwa kama nchi ambayo inaweza kutatua matatizo yake yenyewe”, alisema.

 

Kiongozi huyo wa Coromos alisema Kenya na Comoro zinafanana mambo mengi katika utamaduni na biashara, akisema nchi hizo mbili zitaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

”Kenya inaendelea kuhamasisha nchi nyingi kama zetu, kwa hivyo unaweza kututegemea,” alisema.

Aliziomba nchi za Afrika kukataa mgawanyiko na kufanya kazi kwa ajili ya maisha ya watu na kuboresha fursa kwa ajili yao.

”Tunahimiza mazungumzo kwa ajili ya utatuzi wa amani, nadhani tunaweza kufanya kazi ili kukabiliana na vikwazo hivi ili kujenga maisha bora ya baadaye,” alisema.

 

”Hii ni fursa kwetu, ikiwa tutafanya kazi pamoja na kuwajibika kwa watu wetu na kuhifadhi maadili yao.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!