Home » Atwoli Apuulizia Kushurutisha Wafanyikazi Kuunga Mswaada Wa Nyumba

Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli amepuuzilia mbali ripoti za vyombo vya habari kwamba wafanyikazi wa Kenya walikuwa na mzozo kuhusu mapendekezo ya ushuru wa nyumba uliopendekezwa na rais William Ruto.

 

Katika taarifa ya hii leo Jumatano mkuu huyo wa COTU amebaini kuwa ripoti hizo ni za uongo na suala hilo lilikuwa tayari limekamilika.

 

Zaidi ya hayo, chama hicho kikuu cha wafanyakazi kimebainisha kuwa hakukuwa na majadiliano kuhusu miradi ya nyumba za bei nafuu wakati wa mkutano uliyokamilika hivi majuzi mjini Kisumu mnamo Mei 23.

 

Hata hivyo ripoti inayozungumziwa imebainisha kuwa mdadisi wa ndani katika chama hicho alifichua kwamba mwanaharakati huyo mkongwe wa vyama vya wafanyakazi alikutana na wanachama ili kuwashurutisha kuunga mkono mswada huo.

 

Hii ilikuwa baada ya muungano huo kukosa kutoa mapendekezo yoyote kuhusu mswada huo wakati wa mikutano ya hadhara.

 

COTU imebaini kuwa habari hizo ni za uongo ikieleza kuwa viongozi wote wa muungano huo wanamuunga mkono kikamilifu katibu mkuu kuhusu suala hilo.

 

Mwanachama huyo wa chama cha wafanyakazi mnamo Mei 8, aliwakashifu wanachama wa chama hicho na watumishi wa umma kwa kupinga ushuru wa nyumba akieleza kuwa walishindwa kuhudhuria mkutano na rais ambapo suala hilo lilijadiliwa na kuhitimishwa.

 

Ameonya dhidi ya kuingiza siasa katika suala hilo akiwataka kukumbatia mazungumzo ya kijamii.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!