Home » Bungoma: ‘Nabii Yohana Wa Tano’ Kujiwalisha Kwa Polisi

Kamanda wa polisi wa Bungoma, Francis Kooli amemwagiza Nabii Yohana wa tano, anayejiita kiongozi wa kanisa la ‘Muungano For All Nations’ lililopo katika kijiji cha Nandolia, Kanduyi Kaunti ya Bungoma kufika katika afisi zake tarehe mbili mwezi ujao.

 

Nabii Yohana wa Tano ambaye jina lake halisi ni Geoffrey Wanyama Nakalila ameoa wake 42, huku mdogo akiwa na umri wa miaka 24 Yohana, mwenyewe ana umri wa miaka 83, ana watoto 289.

 

Kamanda wa polisi amemwomba Nabii afike ofisini kwake tarehe 2 Juni kwa mahojiano.

 

Nabii Yohana wa Tano ameunda Biblia yake yenye vitabu 93, ambayo ni kinyume na Biblia Takatifu ya kawaida ambayo ina vitabu 66 pekee.
Zaidi ya hayo, pia ameanzisha amri 12 badala ya amri 10 za jadi zilizopitishwa na Musa wa Biblia.

 

Hili limezua ghasia mjadala miongoni mwa wenyeji, huku wengine wakitaka Nabii akamatwe kwa mafundisho yake na kutilia shaka Biblia ambayo ilikuwa imeandikwa naye.

 

Wenyeji wameibua wasiwasi iwapo Biblia na shughuli za kidini za Nabii ziliafiki viwango vya katiba ya Kenya kulingana na sheria ya Vitabu na Magazeti.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!