Wakenya Walalamikia Malipo Ya NHIF
Hisia balimbali zimeenea mtandaoni baada ya Wakenya kadhaa kulalamika kuhusu Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) kuondoa asilimia mbili ya bili zao za hospitali licha ya kulipia kila mara.
Hali imeendelea kuwa mbaya zaidi ambapo mtumiaji mmoja wa mtandaoni aliyetambuliwa kama Abdul alionyesha kuwa kujifungua kwa mkewe kuligharimu Ksh87,000 na kushangaa kwa nini Hazina ilijitolea kulipia kitanda cha siku tatu pekee ambacho kilifikia Ksh3,000.
Kwa kujibu, NHIF imefafanua kuwa walitoa aina mbili za bili za hospitali zinazojumuisha malipo ya kina yaani comprehensive.
Katika hali nyingine, mazungumzo yameelekea kwa Hazina ya kulipa tu huduma za malipo ya juu kwa wafanyikazi wa umma na kuwatenga Wakenya wengine.
Mshauri wa Utawala Omore Osendo ameangazia kuwa babake aliulizwa ikiwa yeye ni mfanyakazi wa umma kupata huduma fulani licha ya kulipa michango kwa zaidi ya miongo mitatu.
Aidha Hospitali zimepangwa katika makundi mawili; Wanachama wa Mpango wa Kitaifa wa Afya (N.H.S) na Mpango Ulioboreshwa (E.S).
N.H.S ambayo inajulikana zaidi kama Universal Health Care Supercover, ndiyo bima ya msingi ya afya kwa wanachama wote na wategemezi wao.
Hata hivyo bima hiyo Inajumuisha Wakenya walioajiriwa na ambao wametimiza umri wa miaka 18.
Kwa upande mwingine, E.S inashughulikia watumishi wa umma, Polisi wa Kitaifa, serikali za Kaunti, mashirika ya umma na mipango ya pensheni kwa maafisa wa umma waliostaafu.
Jinsi ya Kuangalia Orodha ya Hospitali Zote Zinazoshughulikia Kikamilifu na Isiyo Kikamilifu
Nenda kwenye ukurasa rasmi wa NHIF: nhif.or.ke
Bofya aikoni ya Wanachama na ubofye kategoria ya orodha ya hospitali.
Chagua kati ya NHS na ES na ubofye aikoni zozote ili kuona aina husika ya hospitali.
Chini ya mpango, bofya aikoni husika au jina la kategoria za hospitali ili kufungua orodha ya jedwali.