Home » KRG Kwa ‘Binti Wake’: Nilikuwa Katika Darasa La 6 Ulipozaliwa

KRG Kwa ‘Binti Wake’: Nilikuwa Katika Darasa La 6 Ulipozaliwa

Msanii wa dancehall wa Kenya na mfanyabiashara KRG the Don amesisitiza kuwa anaamini yeye sio baba wa Yvonne Njoki wa miaka 19.

 

KRG na Yvonne walikutana jana na kufanya mazungumzo ambapo alisisitiza kwamba bado alikuwa katika Shule ya Msingi mwaka ambao Yvonne alitungwa mimba.

 

“Mwaka 2002 nilikuwa na umri wa miaka 11, hakuna jinsi mimi ni baba yako, wewe ulizaliwa 2003 hivyo haiingiani, mimi nilikuwa darasa la sita mwaka huo, wenzangu wanaweza kushuhudia hilo na mimi sikuwa Nairobi wakati huo.”

 

Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa mwaka wa 2002 alikuwa Kilgoris na si Nairobi kama mamake Yvonne alivyodai.

 

KRG  alisema kwa ajili ya Yvonne yuko tayari kuendelea na mtihani wa uzazi kwa kuwa kama mzazi anaelewa jinsi ilivyo ngumu kwa mtoto kukua bila kujua wazazi wake.

 

Mamake Yvonne alidai alikutana na KRG the Don alipokuwa mdogo na alikuwa akifanya kazi Gikomba.

 

Alieleza kuwa KRG alikubali ujauzito huo na hata kumtunza mtoto kwa miezi michache ya kwanza kabla ya kukutana na msichana mwingine na kuwatelekeza.

 

Alidai KRG alizaliwa miaka ya 80 na sio 1992 kama asemavyo.

 

Mwanamuziki huyo alisisitiza kuwa alipata kitambulisho chake mwaka wa 2010 na hajawahi kukutana na mamake Yvonne.

 

Hata hivyo aliahidi kuwa iwapo matokeo ya DNA yatakuwa sawa nayeye, ataomba msamaha na kuanza kuwajibika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!