Home » Kundi La Kanini Kega Lafichua Uongozi Mpya Wa Jubilee

Mrengo wa Jubilee unaoongozwa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kanini Kega umebaini kuwa uko tayari kunyoosha masuala ya Chama cha hicho baada ya kukutana na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

 

Katika taarifa, Aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu amedokeza kura ya maamuzi inayokuja kubaini ni mrengo gani kati ya unaoongozwa na Kega unaounga mkono utawala wa Rais William Ruto, na mwingine unaoongozwa na Jeremiah Kioni utadhibiti chama hicho.

 

Wambugu amefichua kuwa Jubilee ina mirengo miwili ndani yake Jubilee ya Azimio ambayo amedai ilikuwa imekwama siku za nyuma na Jubilee Kenya ambayo inaunga mkono Urais wa William Ruto.

 

Haya yanajiri baada ya mkutano uliohusisha wabunge 11 wa zamani kutoka Bunge la kumi na mbili kutoka eneo la Mlima Kenya waliokutana na Gachagua katika makazi rasmi ya naibu rais Karen.

 

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Kieni Kanini Kega, aliyekuwa mbunge wa Kiambu mjini Jude Njomo na aliyekuwa mbunge wa Othaya James Gichuki.

 

Kwa upande mwingine, naibu rais Gachagua amewapongeza kwa kuunga mkono utawala wa Kenya Kwanza hata baada ya kupoteza viti vyao vya Ubunge.

 

Mnamo Mei 23, Wambugu alimkashifu aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwahadaa watu wa Jubilee na kukosa kuonyesha uongozi.

 

Aidha Chama cha Jubilee kimekumbwa na mvutano na vuta nikuvute kati ya aliyekuwa Mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Kioni na aliyekuwa Mbunge wa Kieni Kanini Kega, wote wanaodai kuwa ndio Katibu Mkuu halali wa chama hicho (SG).

 

Zaidi ya hayo, Rais msaatu Uhuru Kenyatta, ambaye ni mwenyekiti wa Jubilee, anapigania kiti chake huku mbunge mteule Sabina Chege akidai kuwa mwenyekiti.

 

Mnamo Februari 4, Kega na mwenyekiti wa Jubilee Nelson Dzuya waliwasimamisha kazi Kioni na David Murathe baada ya mkutano wa Kundi la Wabunge mjini Nakuru.

 

Mnamo Mei 22, Uhuru aliongoza Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa Chama cha Jubilee (NDC) katika uwanja wa Ngong’ Racecourse ambapo aliwatimua wanachama kumi wa chama hicho akiwemo anayedaiwa kuwa mrithi wake Sabina Chege na Kega.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!