Home » Naibu Mwenyekiti Wa UDA Seth Panyako Ajiuzulu

Naibu Mwenyekiti wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Seth Panyako amejiuzulu wadhifa wake katika chama tawala ambacho kiko katika muungano wa Kenya kwanza.

 

Afisa huyo wa zamani wa chama amedokeza kuwa anajiuzulu kutoka kwa chama hicho baada ya kupinga mapendekezo ya Hazina ya Makazi yaliyotetewa na Rais William Ruto.

 

Kulingana naye wazo hilo halijawaridhisha baadhi ya Wakenya ambao wanahangaika kujikimu kimaisha.

 

Panyako ambaye pia anahudumu kama Katibu Mkuu wa Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi Kenya (KNUN) ametaja gharama ya juu ya maisha kuwa chanzo chake kugura chama hicho ambapo anadai inaonekana muungano wa Kenya hauko tayari kumsikiliza mkenya wa kawaida huku wengi wakifa njaa bila msaada.

 

Aidha, afisa huyo wa zamani wa chama ameonyesha kutokubaliana na hazina ya nyumba katika siku za hivi karibuni.

 

Hata hivyo, amesema Serikali lazima iwe na ubunifu wa kutosha kuwa na rasilimali za kufanya mradi huowa nyumba huku akihoji kwamba Kwa nini hawawezi kutumia fedha ambazo tayari zipo kufanya Mradi huo wa nyumba za bei nafuu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!