Waliokuwa Wabunge Wa Jubilee Wagura Azimio
Naibu Rais Rigathi Gachagua hii leo Jumamosi amewakaribisha waliokuwa Wabunge wa Chama cha Jubilee kutoka mlima Kenya ambao walionyesha kuunga mkono kikamilifu utawala wa Kenya Kwanza.
Gachagua amefanya mashauriano kwa muda mrefu na wabunge walioshindwa katika uchaguzi uliopita katika makazi yake rasmi huko Karen, Nairobi.
Gachagua amesema anashukuru kuwakaribisha wabunge wa zamani aliohudumu nao katika Bunge lililopita na kuongeza kuwa yuko tayari kufanya kazi na yeyote kuhakikisha ufanisi wa serikali ya Rais William Ruto.
Aidha Wabunge hao wa zamani, ambao wamekuwa wakosoaji vikali wa utawala wa rais Ruto na kumuunga mkono mgombeaji urais wa muungano wa Azimio Raila Odinga katika kura za mwisho, wamemweleza Naibu Rais kuwa wamekubali kwamba Rais alishinda kwa haki na wako tayari kuweka uzito wao nyuma ya utawala tawala.
Mkutano wa Jumamosi ulikuwa ni nyongeza ya azma ya naibu rais ya kuhakikisha viongozi hawaachwi nyuma katika maendeleo ya maeneo mbalimbali kote nchini.
Kulingana na Gachagua ana nia ya kukumbatia kila mtu licha ya tofauti za kisiasa zilizopita huku wakitekeleza Mpango wa mageuzi wa Kenya Kwanza.
Viongozi hao wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Jubilee Kanini Kega walijitenga na maandamano ya Muungano wa Azimio na kujaribu kufufua kundi hatari la Mungiki shughuli zinazofanywa na baadhi ya viongozi katika eneo hilo.
Viongozi hao hata hivyo wameahidi kuheshimu matakwa ya wapiga kura katika uchaguzi uliopita na kuunga mkono viongozi waliochaguliwa kuwatumikia wananchi.