Home » Mkurugenzi Mkuu WA KEBS Wengine 7 Washtakiwa Kwa Kuiba Sukari

Mkurugenzi Mkuu WA KEBS Wengine 7 Washtakiwa Kwa Kuiba Sukari

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini (KEBS) Benard Njiraini na wenzake saba wamekanusha shtaka la uhalifu la kuiba sukari ya yenye thamani ya Sh20 milioni.

Washtakiwa wamefikishwa mbele ya mahakama ya Nairobi Milimani ambapo wamekanusha kosa hilo na kuachiliwa kwa thamana ya pesa taslimu Sh400,000 kila mmoja.

 

Washtakiwa hao kwa mujibu wa upande wa mashtaka wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya tarehe 9 Desemba 2022 na Mei 3, 2023.
Bidhaa hiyo ilikusudiwa kutumiwa katika kutengenezea ethanoli ya viwandani na Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA).

 

Kiongozi huyo ameshtakiwa pamoja na Joseph Kiagu, Derrick Njeru, Peter Njoroge na Crispus Waithaka.

 

Washtakiwa wengine ni pamoja na Mohammed Hassan, Abdi Yusu na Pollyanne Njeri.

 

Kulingana na upande wa mashtaka bidhaa hiyo iligunduliwa go-down eneo la Makongeni mjini Thika kati ya tarehe 21 Aprili 2023 na Mei 3, 202.

 

Mahakama imeamuru kwamba kesi hiyo itajwe Juni 6 kwa madhumuni ya mkutano wa kabla ya kusikilizwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!