Home » Mr Seed Arejea Studioni

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Mr Seed amerejea studio na kutengeneza wimbo mpya na rafiki yake wa karibu na mwanamuziki Bahati wiki kadhaa baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani iliyogharimu maisha ya mpiga picha wake, Ambroze Khan.

 

Katika video inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, mwimbaji huyo anayeonekana kuimarika anaonekana studio akiimba wimbo pamoja na Bahati.

 

Ajali hiyo iliyotokea Jumamosi ya Aprili 29,

 

Kulingana na mkewe Nimo, walikuwa wakielekea kwa shughuli za kununua ardhi huko Nanyuki tukio hilo la kusikitisha lilipotokea.
Ameongeza kuwa mumewe alibahatika kuwa hai na anamshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake.

 

Mwanzilishi wa studio za Starborn Empire alilazimika kupumzika kwa kitanda kwa wiki tatu na akachagua kuchukua mapumziko kwenye mitandao ya kijamii ili kumpatia muda wa kupona.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!