Home » DCI Kooni Mwa Mchungaji Ezekiel

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) inaomba mahakama iongezee amri ya kufungia akaunti za benki za mchungaji Ezekiel Odero ikisema kuwa uchunguzi katika akaunti za benki hizo ni tata.

 

Siku za awali zilizotolewa na mahakama kufungia akaunti za benki za mchungaji huyo ziliisha jana Jumapili, hata hivyo, mahakama iliziongeza hadi hii leo Jumatatu.

 

Sasa, DCI inataka siku saba zaidi kuruhusu kampuni ya Safaricom kutii maagizo ya mahakama iliyotolewa mapema mwezi huu.

 

Mahakama imeambiwa kuwa uchunguzi kuhusu akaunti ya benki ya kasisi Ezekiel Odero haujakamilika, huku wapelelezi wakiilaumu Safaricom kwa kutotii maagizo ya mahakama.

 

DCI, kupitia afisa wa uchunguzi sasa anataka Safaricom iitwe kufika mahakamani kueleza ni kwa nini hawajatii maagizo ya mahakama.
Mchungaji Ezekiel Odero anachunguzwa kuhusu madai ya utakatishaji fedha na uhalifu wa kiuchumi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!