Ifahamu Flower Three Ya Rayvanny
Imeshazoeleka ya kuwa muendelezo wa kazi nyingi za muziki pamoja na filamu umekuwa ukifanywa na nchi zilizoendelea. Mabadiliko ya sasa ni baada ya mwanamuziki Rayvanny kuachia kazi ya tatu mfululizo aliyoipa jina la Flower three.
SOMA PIA:Rayvanny Azidi Kunogewa na Penzi La Fahyma Kwenye Forever
Ujio wa Flower Three ni muendelezo wa Extended Playlist za mshindi huyo wa tuzo za BET. Baada ya kuachia Flower one mwaka 2019 pamoja na Flower two iliyotoka mwaka 2022 na sasa kuamua kuja na kazi nyindine mwaka huu wa 2023.
Ukali wa kazi hiyo ya tatu umejumuisha jumla ya nyimbo tisa ambazo kati ya nyimbo hizo kuna baadhi ya nyimbo alizoshirikisha wasanii wenza. Nyimbo hizo ni kama vile Dance aliyoifanya na Jay Melody, Mchepuko akimshirikisha Phina, Mwambieni aliyoifanya na mwanamuziki wa NLM Macvoice pamoja na Mtamu ikiwa ni kazi aliyoifanya na mwanamuziki kutoka Kenya Bahati.
Mfululizo wa kazi za Flower umekuwa ukibeba jumbe za Mahaba. Huba linalongelewa katika EP ni Penzi tamu licha ya ngoma ya Mchepuko kuwa na ujumbe wenye ukakasi tofauti na zingine.
Rayvanny katika ngoma zote tisa katika Extended Playlist ya hiyo, ni ngoma tatu pekee mpaka sasa alizofanikiwa kuachia Video rasmi. Video hizo ni pamoja na Forever, Mchepuko pamoja na Habibi.
Huu ni utamu mwingine wa kazi zenye ladha ya Bongo Fleva huku matumizi ya lugha ya Kiswahili yakitaradadi kwa upana. Matumizi ya maneno kama Habibi yakinogesha upekee wa nyimbo za EP hiyo ya Chui.