Home » Gachagua Aapa Kuondoa Mashirika Na Madalali Katika Uzalishaji Wa Kahawa

Gachagua Aapa Kuondoa Mashirika Na Madalali Katika Uzalishaji Wa Kahawa

Naibu Rais Rigathi Gachagua leo hii Ijumaa ameahidi kuondoa walaghai katika sekta ndogo ya kahawa na kushirikiana na washikadau kutatua changamoto zinazoathiri mapato ya wakulima.

 

Gachagua amesema serikali itashughulika kwa uthabiti na madalali yaani (bulkers) katika uzalishaji wa kahawa ili kuboresha hali ya wakulima.

 

Akizungumza katika Shule ya Sekondari ya St. Benedict Wamutitu iliyoko Mukurweini, Kaunti ya Nyeri, baada ya kuzindua basi la shule, Gachagua amesema ameitisha kongamano la siku tatu la washikadau wa kahawa mjini Meru ili kukabiliana na changamoto zinazokumba sekta hiyo.

 

Basi hilo lilinunuliwa kupitia Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Eneo Bunge la Mukurweini (NG-CDF).

 

Kulinagana na naibu rais kongamano la kahawa litafanyika Meru kuanzia Juni 6 hadi 8, 2023 na washikadau wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na maafisa wa serikali, wabunge, Magavana, wakulima wa kahawa, wataalam kati ya watu wengine.

 

Mnamo Januari, Rais Ruto alimpa Naibu Rais jukumu la kuongoza mageuzi ya sekta ya kahawa yaliyoongozwa na Kamati ya Kudumu ya Utekelezaji wa Marekebisho ya Sekta Ndogo ya Kahawa.

 

Viongozi walioandamana na Naibu Rais ni Naibu Gavana wa Nyeri David Kinaniri na wabunge Wambugu Wainaina wa (Othaya), Njoroge Wainaina wa (Kieni), Jane Kagiri wa (Mwakilishi wa Wanawake wa Laikipia), Patrick Munene wa (Chuka Igamba-Ng’ombe) na Dkt Robert Pukose wa (Endebess) .

 

Kuhusiana na oparesheni inayoendelea kufanywa na serikali dhidi ya pombe haramu katika eneo la Kati mwa Kenya, viongozi hao wamepongeza zoezi hiloNaib na kuwataka machifu na wasaidizi wao kuweka juhudi zaidi ili kukabili biashara hiyo haramu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!