Home » Meru Shuttle Yajibu Madai Ya Wafanyakazi Wake Kumvua Nguo Abiria

Meru Shuttle Yajibu Madai Ya Wafanyakazi Wake Kumvua Nguo Abiria

Maafisa kutoka kaunti ya Meru wa kampuni ya Luxury shuttle wamejitokeza kufafanua kuhusu madai kwamba wafanyakazi wao walimvua abiria wa kike kutokana na mzozo wa nauli.

 

Hii ni baada ya picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii za abiria akiwa hana nguo kwenye moja ya magari lao.

 

Ilidaiwa kuwa ‘mwanamke huyo’ anayesemekana kuwa kiziwi alivuliwa nguo kutokana na kushindwa kulipa nauli ya Ksh elfu 1,000.

 

Hata hivyo, katibu wa kampuni hiyo Dan Kanyamu amesema tukio hilo liliingizwa propaganda nyingi na wapinzani wao kibiashara.

 

Huku akikiri kuwepo kwa tukio hilo, amesema abiria huyo ni mwanaume na wala si mwanamke.

 

Kanyamu amesema abiria huyo alipanda gari hilo mwendo wa saa nane usiku katika mji wa Meru na kulala usingizi wakati wa safari ya kuelekea Nairobi.

 

Kulingana naye, waliripoti suala hilo kwa maafisa wa uchunguzi wa CID na maafisa wa uhalifu kwa uchunguzi zaidi.

 

Kesi hiyo bado inaendelea katika Kituo cha Polisi cha Kaunti Ndogo ya Imenti Kaskazini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!