Home » Nakuru: Maafisa Saba Wa Polisi Kulihojiwa Kuhusu Hongo

Maafisa saba wa polisi katika Kaunti ya Nakuru wanachunguzwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusu madai ya kuchukua hongo.

 

Maafisa hao wanasemekana kuomba hongo ili kuachilia gari lililozuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Nakuru.

 

Maafisa walio chini ya uchunguzi unaoendelea ni pamoja na Inspekta Mkuu Derrick Nyaga, Stephen Muinde, Sajenti Jessy Nyamwange, Inspekta Christine Orina, Koplo Jane Wanjiru, Koplo Benjamin Kiptoo Ego, na Konstebo Katito.

 

Uchunguzi unasemekana ulianza baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa dereva akidai kusimamishwa bila sababu kwa tuhuma za ukiukaji wa sheria za barabarani.

 

Mlalamishi alidai maafisa wa polisi waliokuwa wakisimamia kizuizi hicho walidai Ksh.5,000 kutoka kwa dereva na aliposhindwa kutoa, maafisa hao walimkamata dereva pamoja na gari hilo.

 

Maafisa wawili ambao ni Koplo Benjamin Kiptoo Ego almaarufu Jicho Pevu na Stephen Muinde walisindikiza gari hilo hadi Kituo Kikuu cha Polisi cha Nakuru ambako lilizuiliwa na dereva kuwekwa kizuizini.

 

Aidha Dereva alikaa kizuizini hadi siku iliyofuata tarehe 4 Mei 2023 alipoachiliwa baada ya kiasi kilichodaiwa cha Ksh.8,000 kulipwa kwa afisa Jessy Nyamwange, Afisa anayesimamia nidhamu katika Kituo hicho.

 

Dereva anadai maafisa hao waliendelea kulizuilia gari hilo huku wakidai kiasi tofauti cha pesa .

 

Gari hilo lilitolewa baadaye baada ya EACC kuingilia kati kwa sasa Washukiwa hao wameitwa na kurekodi taarifa na katika Tume ya EACC.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!