Home » Gachagua Tayari Kuifanya UDA Vuguvugu La Kitaifa

Gachagua Tayari Kuifanya UDA Vuguvugu La Kitaifa

Naibu Rais Rigathi Gachagua anasema kwamba uongozi wa Kenya Kwanza umejitolea kuhakikisha ushirikishwaji katika kufanya maamuzi kwa kuwezesha ushirikiano na mashauriano endelevu.

 

Akizungumza alipokuwa akiwashirikisha waratibu wa Kaunti 47 wa chama cha (UDA) jijini Nairobi Alhamisi, naibu rais amewataka waratibu na viongozi kushauriana na wawakilishi wa mashinani ili kuhakikisha chama hicho kinakua na kubaki imara kinapotekeleza Mpango wa Kenya Kwanza.

 

Aidha amewataka viongozi waliochaguliwa kuwa washauri zaidi wanapofanya maamuzi.

 

Gachagua pia amesema kuwa hata kama serikali ya Kenya Kwanza inafanya kazi bila kuchoka kutekeleza “Mipango mbalimbali”, pia watahakikisha utawala bora katika sekta zote na majukumu ya uongozi.

 

Akiwa naibu kiongozi wa chama tawala, naibu rais anasema kuwa kila chama cha kisiasa kinaruhusiwa kisheria kuuza ajenda zao kwa Wakenya bila vitisho.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!