Home » Maandalizi Ya Mashindano Ya Raga Yakamilika Mjini Nakuru

Maandalizi Ya Mashindano Ya Raga Yakamilika Mjini Nakuru

Maandalizi ya toleo la 30 la mashindano ya raga ya Great Rift 10 yamekamilika kabla ya hafla hiyo itakayoandaliwa wikendi hii Nakuru Athletic Club.

 

Timu nane ambazo ni pamoja na KCB, Main Machine, na Timu ya Raga ya Nakuru, zimethibitisha ushiriki wao.

 

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya wachezaji 15, Kenya Simbas pia itacheza na Goshawks ya Zimbabwe katika uwanja uo huo kuanzia saa kumi jioni, Jumamosi katika mfululizo wa Kombe la Currie.

 

Timu ya taifa ilirejea Nchini wiki hii baada ya ziara ya mwezi mzima nchini Afrika Kusini na Namibia ikishiriki katika Mechi za Daraja la Kwanza za Kombe la Curry.

Mechi dhidi ya Zimbabwe itakuwa ya kwanza kati ya mechi tatu ambazo Kenya itacheza nyumbani katika msururu huo.

Kocha Msaidizi wa Simbas ya Kenya, Curtis Olago, ameeleza kujiandaa kwa kikosi kuelekea mechi ya Jumamosi.

 

George Ambua, amesema timu hiyo itatumia pambano hilo kujipima na kusaidia kuijenga upya Simba na kuongeza kuwa wanaisubiria kwa hamu mechi hiyo ikiwa katika kiwango cha juu.

 

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Michezo ya Kaunti ya Nakuru, Josephine Achieng, amewataka mashabiki na wafuasi wa raga kujitokeza kwa wingi akisema wanalenga jumla ya watu 5,000 kuhudhuria tamasha hilo la siku mbili la michezo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!