Home » Watoto 17 Waripotiwa Kutoweka Nchini Kenya Kila Siku

Wakati ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha siku ya kimataifa ya watoto waliopotea, takwimu zimeonyesha kuwa takriban watoto elfu 6,500 hupotea kila mwaka nchini Kenya ambayo ni sawa na watoto 18 kila siku.

 

Maafisa wa Polisi wanasema idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi ikizingatiwa kwamba watoto wengi zaidi waliopotea hawaripotiwi kamwe.
Polisi sasa wanawataka wananchi kuripoti watoto waliopotea ili kupata takwimu zinazofaa.

 

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Missing Child Kenya Foundation Mary Munyendo, amethibitisha kwamba wengi wa watoto walioripotiwa kupotea walisafirishwa nje ya nchi kisiri.

 

Kamishna Msaidizi wa Polisi Wilkister Nyaiwo kwa upande wake alitoa wito kwa kila mtu, wazazi na wasio wazazi kushiriki katika kuhakikisha watoto waliopotea wanapatikana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!