Home » Waziri Aongoza Hafla Ya Kufuzu Kwa Askari Wa Akiba Baringo

Waziri Aongoza Hafla Ya Kufuzu Kwa Askari Wa Akiba Baringo

Hali ya wasiwasi imetanda katika eneo la Loruk huko Baringo Kaskazini baada ya majambazi kuvamia na kumpiga risasi mtu mmoja na kumjeruhi vibaya.

 

Zaidi ya ng’ombe mia 300 waibiwa wakati wa tukio hilo na kuelekezwa milima ya Paka huko Tiaty.

 

Majambazi hao waliokuwa na silaha hatari walishambulia majira ya saa 12 mchana jana Jumatano wakati ng’ombe hao wakichunga malishoni.

 

Maafisa wa Polisi waliokabiliana na majambazi hao katika mashambulizi hayo walizidiwa nguvu huku majambazi wakifanikiwa kuondoa mifugo hao.

 

Uvamizi huo tangu wakati huo umewalazimu wakaazi wa Tiaty wanaoishi Loruk kufunga maduka kwa kuhofia mashambulizi ya kulipiza kisasi.

 

Uvamizi huo unajiri kufuatia maombi ya muda wa siku 5, mpango wa mke wa rais Rachel Ruto, unaolenga maombezi ya kurejesha amani katika kaunti sita ambazo zimetangazwa kukosa usalama.

 

Aidha, Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki leo amefika eneo hilo na kusimamia gwaride la askari wa akiba mia 200 waliokuwa kwenye mafunzo kwa muda wa wiki mbili zilizopita.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!