Home » Wafanyabiashara Kariakoo Waendeleza Mgomo

Wafanyabiashara Kariakoo Waendeleza Mgomo

 

Wafanyabiashara wa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam wameendeleza mgomo wao wa kutokufungua maduka na leo ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa mgomo huo siku ya Jumatatu.

 

SOMA PIA:Anerlisa Atoa Onyo Kali Kwa Wafanyabiashara

 

Katika mgomo huo wafanyabiashara hao walilalamikia kero ya kodi inayotozwa na mamlaka ya mapato TRA ndiyo iliyoshutumiwa kwa kodi hizo ambazo zimepelekea kutia mgomo.

 

 

Licha ya kuwa Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kuwasili sokoni hapo siku ya Jumatatu na kuwasihi wafanyabiashara kufungua maduka, lakini bado wamekazia mgomo huo kwa kutokufungua maduka yao.

 

Siku ya Jumatano mkutano wa Wafanyabiashara hao unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo wafanyabiashara hao watakutana na Waziri mkuu kwa ajili ya kusikiliza changamoto zao pamoja na kuzitatua.

 

Soko la Kariakoo ni moja kati ya masoko makubwa ambayo yamekuwa kitovu cha biashara kwa wafanyabiashara wa ndani ya Tanzania na hata nje ya nchi hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!