Yanga Mabingwa Ligi Kuu NBC
Klabu ya soka ya Young Africans sports club wameibuka washindi wa ligi kuu ya Tanzania bara mara baada ya mchezo wake dhidi ya Dodoma Jiji, katika mchezo ambao Yanga walishinda bao 4-2.
SOMA PIA:Yanga, Simba Waendeleza Ubabe Ligi Kuu Ya Tanzania
Mabao hayo ya ushindi kwa klabu ya Yanga yalitiwa nyavuni na Mudathir Yahya, Farid Mussa pamoja na Kennedy Musonda aliyefunga mabao mawili katika uwanja wa Azam complex Chamazi.
Yanga wameweza kutetea ubingwa wao na utakuwa ubingwa wa 29 wa klabu hiyo huku wakibakiza michezo miwili ambao ni mchezo wa Mbeya city pamoja na ule wa Tanzanian prison.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa klabu hiyo ambayo msimu uliopita pia waliibuka washindi wa ligi hiyo na sasa mchezo unaofuata ni kati ya Yanga dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya nusu fainali ya mzunguko wa pili.