Home » Mkutano Wa Wazazi Mukumu Girls Watibuka

Maafisa wa Polisi Jumapili walilazimika kutumia vitoa machozi baada ya mkutano wa wazazi Shule ya Upili ya Wasichana ya Mukumu kugeuka kuwa uwanja wa mapigano .

 

Wazazi hao walikuwa wameandamana na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale na Mwakilishi wa Wanawake Elise Mukhanda ambao walishutumu shule hiyo kwa kuhifadhi chakula ambacho si salama kwa matumizi.

 

Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa Jumanne baada ya kufungwa wiki tatu zilizopita kufuatia mkurupuko wa ugonjwa ambao umesababisha vifo vya wanafunzi watatu na mwalimu mmoja.

 

Mwishoni mwa Machi, wanafunzi 72 kutoka shule hiyo yenye makao yake makuu katika Kaunti ya Kakamega walilazwa katika Hospitali Kuu ya Kaunti ya Kakamega, huku maafisa wa afya wakishuku kuwepo kwa ugonjwa wa Kipindupindu.

 

Maafisa wa afya wa kaunti, hata hivyo, waliondoa uvumi wa ugonjwa wa Kipindupindu baada ya vipimo kufichua uwezekano wa sumu ya chakula.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!