Sakaja Adai Maelewano Kati Ya Azimio Na Kenya Kwanza
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametaka mzozo wa Azimio na Kenya Kwanza kusuluhishwa haraka iwezekanavyo.
Sakaja akizungumza katika kanisa la PCEA Umoja, ambapo alikuwa amehudhuria ibada pamoja na Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli,amewahakikishia wakazi wa jiji hilo usalama wao iwapo maandamano ya kuipinga serikali yataendelea.
Muungano wa Azimio ulitoa wito wa kuanzishwa tena kwa maandamano dhidi ya serikali Jumanne, Mei 2 baada ya mazungumzo ya pande mbili kusambaratika wiki jana.
Mazungumzo hayo yalidorora huku wajumbe wa kamati ya pande mbili wakitofautiana kuhusu kujumuishwa kwa mbunge Keynan na mwenzake wa Pokot Kusini David Pkosing, suala ambalo walisema ni lazima litatuliwe kabla ya shughuli rasmi kuanza.
Viongozi wa Azimio waliwashutumu wenzao wa Kenya Kwanza kwa upotovu wakisisitiza kuwa kujumuishwa kwa Keynan katika timu ya mazungumzo ya Kenya Kwanza ilikuwa kinyume cha sheria tangu alipochaguliwa kwa tikiti ya Jubilee, chama tanzu cha Azimio.
Kenya Kwanza kwa upande mwingine ilisema chama cha mbunge David Pkosing cha KUP kilikuwa kikihusishwa na muungano unaotawala hatua ambaye kwa sasa Kenya kwanza imemtoa Keynan kama mmoja wa wajumbe wake..