Mvua Bora Huchangia Umeme Nafuu, KenGen Yasema
Afisa mkuu mtendaji wa KenGen Abraham Serem ametangaza kuwa viwango vya maji katika mabwawa makubwa vitahakikisha kuwa kuna uzalishaji wa kutosha wa umeme.
Serem amesema nchi imerekodi viwango vya chini vya maji katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Serem, ambaye pia ni kaimu mkurugenzi mkuu wa KenGen, amezungumza wakati wa uzinduzi wa upanzi upya wa msitu wa Gathiuru katika kijiji cha Burguret eneo bunge la Kieni, Kaunti ya Nyeri.
Katibu Mkuu wa Kawi Alex Kamau Wachira kwa upande wale alisema wizara yake inalenga kutii lengo la Rais William Ruto la kuhakikisha nchi inafikia misitu bilioni 15 katika miaka 10 ijayo.