Home » Zuchu Avunja Rekodi Golden Club Boomplay

 

Mwanadada anayetamba na vibao mbalimbali vyenye ladha ya baibuda kama vile Napambana pamoja na Raha, Zuchu, amefikia rekodi mpya katika jukwaa la mziki la  Boomplay mara baada ya kufikia wasikilizaji milioni 200 katika nyimbo zake.

 

SOMA PIA:Mashabiki Wa Zuchu Wafurahishwa Na Tuzo Za Tanzania

 

Hatua hiyo aliyoipiga Zuchu huko Boomplay imechangiwa na Extended Playlist yake ya kwanza ya I am Zuchu ya mwaka 2020 ambayo ndiyo iliyomtambulisha na bila kusahau nyimbo zake maridhawa ikiwemo Sukari, Nyumba ndogo,  bila kusahau mikwaju mingine kama vile Fire, Jaro pamoja na  Love aliyomshirikisha Adekunle Gold Kutokea Nigeria.

 

 

Mbali na Zuchu pia wasanii wengine waliofanikiwa kuingia Golden Club Boomplay ni pamoja na Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize bila kumsahau mkali wa ngoma ya Mahaba Ali Kiba.

 

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa amekuwa kimya kidogo kutokana na mfungo wa Ramadhani anatarajiwa kurejea kwa kazi pambe baada ya kuwaacha mashabiki zake na ukata wa nyimbo kwa muda mrefu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!