Home » Otiende Amolo, Gitonga Murugara Kuongoza Mazungumzo Ya Pande Mbili Ya Bunge

Otiende Amolo, Gitonga Murugara Kuongoza Mazungumzo Ya Pande Mbili Ya Bunge

Uongozi wa bunge kutoka miungano ya Azimio la Umoja na Kenya Kwanza umeamua mbunge wa Rarieda Otiende Amollo na mbunge wa Tharaka George Murugara kuongoza kamati ya mazungumzo ya pande mbili.

 

Wabunge hao wawili wataongoza timu inayojumuisha viongozi Ledama Ole Kina, Edwin Sifuna, Enoch Wambua, Amina Mnyanzi, Millie Odhiambo, David Pkosing ambao ni wa (Azimio) na Boni Khalwale, Hillary Sigei, Esther Okenyuri, Mwengi Mutuse, Adan Keynan na Lydia Haika ambao ni wa (Kenya Kwanza).

 

Wakati wa mazungumzo yao ya kwanza ya awali kuhusu mchakato wa mazungumzo ya pande mbili, pande zote mbili zimeibua wasiwasi juu ya orodha ya wabunge waliochaguliwa na kila muungano kuongoza mazungumzo hayo.

 

Aidha, Azimio ina wasiwasi kuhusu Kenya Kwanza ikiwa ni pamoja na Adan Keynan wa (chama cha Jubilee) wa kamati hiyo, wa pili ni kuhusu uamuzi wa Kenya Kwanza kumtaja David Pkosing wa (KUP) kama mwanachama wa kamati hiyo…ambapo azimio inadai kuwa wawili hao walikuwa wanachama wake awali.

 

Hata hivyo, uongozi wa bunge kutoka miungano yote miwili umeazimia kuwa mchakato wa mazungumzo ya pande mbili uendelee, hata kukiwa na mkwamo.

 

Kwa upande wake, kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wa amesema mkutano wa leo Alhamisi unatoa idhini kwa wanachama wa kamati ya pande mbili kushiriki kwa njia yeyote ile.

 

Miongoni mwa masuala ambayo ushirikiano wa pande mbili za bunge utashughulikia ni pamoja na kuundwa upya kwa jopo la uteuzi kuhusu uajiri wa wanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!