Home » Gachagua Aongoza Vita Dhidi Ya Pombe Haramu Mlima Kenya

Gachagua Aongoza Vita Dhidi Ya Pombe Haramu Mlima Kenya

Naibu Rais Rigathi Gachagua ameongoza ujumbe wa serikali kwenye mkutano mkubwa hii leo kama njio moja wapo ya kutafuta suluhu dhidi ya ongezeko  ulevi na pombe haramu.

 

 

Gachagua amesema serikali imeanzisha vita kali dhiti ya vinywaji hivyo na akawahimiza viongozi wote hususan kutoka mkoa wa kati pamoja na vitengo vtote vya usalama kukaza Kamba ili kumaliza ubugiaji wa bombe haramu haswa kwa vijana.

 

 

Gachagua alikuwa akizungumza siku ya Ijumaa mjini Nyeri kwenye mkutano wa kushughulikia suala la unywaji wa pombe haramu ambapo alifichua changamoto za ulevi umechangia pakubwa uvunjikaji wa ndoa, ukosefu wa maadaili, na kupungua kwa kizazi maeneo hayo.

 

 

Alisema haiwezi kuwa wale ambao wamepewa jukumu la kukabiliana na hatari hiyo ndio wanasaidia walanguzi wa dawa za kulevya.

 

 

Gachagua alikuwa ameandamana na viongozi wa juu serikali wakiwemo mawaziri, magavana , wabunge kutoka vitengo vyote vya usalama vikiongozwa na inspekta jenerali wa polisi na viongozi kadha kutoka mlima kenya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!