Home » Nakupenda Yamuingizia Jay Melody 200M+

 

Mwandishi na Mwanamuziki Sharif Said al maarufu kama Jay Melody ambaye kwa sasa bado anavimba na kibao chake cha Sawa amefanya mahojiano na Milard Ayo na kueleleza ya kuwa wimbo wa Nakupenda umefanikiwa kumuingizia zaidi ya shilingi milioni 200 za kitanzania.

 

SOMA PIA:Marioo, Paula Wazama Penzini

 

Katika mahojiano hayo Jay Melody alieleza ya kuwa licha ya kuingiza kiasi hicho cha pesa lakini pia Nakupenda ndio wimbo wake ambao umemtambulisha kwa ukubwa zaidi kati ya nyimbo zake zote ambazo aliwahi kuziachia.

 

 

Katika kuanza mahojiano, Millard alimsifu Jay Melody kwa kujali muda baada ya kufika eneo husika kabla ya muda uliopangwa.  Hili limekuwa suala kubwa kwa nyota wengi nchini Tanzania ambao kutokana na majina yao au umaarufu huchelewa kufika katika mihadi waliyokubaliana na watu.

 

Kwa sasa Jay Melody amezidi kuziteka hisia za mashabiki wengi haswa wanawake kwa kuwavutia zaidi na aina ya uimbaji wake uliojikita katika mapenzi kama  katika nyimbo zake ikiwemo sawa pamoja na Nitasema

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!