Risper Faith Aweka Wazi Mambo Yanayovunja Ndoa
Sosholaiti Risper Faith amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 6 na amepata hekima kuhusu kile kinachosumbua ndoa za leo.
Akishiriki vidokezo vyake kwenye chaneli yake ya YouTube ya Rispers World, sosholaiti huyo aliteta kuwa makosa mengi yanafanywa na wanawake.
“Siku hizi kuna mambo mengi sana yanatokea. Hata mimi ndoa yangu haijakamilika lakini huwezi kuniona nikienda kwenye mitandao ya kijamii kuanika siri zangu,” alijitaja.
“Sema kwa mfano mwenzako anakoroma kitandani, labda anakojoa kitandani, au mdomo wa mwenzio unanuka, mambo kama hayo.Hizo ni siri zako za ndoa hutakiwi kuziweka wazi, kwanini unaziweka wazi? anadai.”
Kuongeza zaidi
“Mama yangu aliniambia ukiwa na tatizo kwenye ndoa yako nipigie tuongee au nenda kanisani ukaongee na Mungu wako.
Lakini usiwaambie watu hata ndugu zako. Imagine kama bwanako anakojoa kwa kitanda uende umekutana na mabeshte zako then unawaambia.
Guess what the next time wakimuona wanampachika jina la kikojozi, ati ndio ule kikojozi amecome.”
“Halafu siku moja Kamau atakuja kugundua kuwa unamtambulisha kwa marafiki zako wa karibu ambao anakojoa.
Akikojoa kitandani usifichue, hiyo ni siri yako ya ndoa, hizo ni vitu kupelekea dakatari awapatie dawa, diapers ama mnunue au chochote unachohitaji kutatua” Alishauri.
Sababu nyingine inayofanya ndoa kushindwa kulingana na Risper ni kueleza kuhusu changamoto zako za kifedha.
“Siri zenyu mzike huko kwa nyumba, usike kwa kaburi lakini usiende kuwaambia wapenzi wako siri zako za ndoa yako, unanisikia?
Watatumia dhidi yako”
Alidokeza kuwa imekuwa mbaya zaidi kwa sababu ya mitandao ya kijamii ambapo marafiki hufichua siri zako
“Na siku hizi kila mtu unajua social media, mtu ata andika online Kamau anakojoanga kitanda so Kamau will be a laughing stock, do you want the father of your child to be a laughing stock? No! “
Risper pia aliwalaumu wanawake kwa kutokuwa watiifu, na kusahau majukumu yao kama walezi wa nyumbani.
Alieleza kuwa anahakikisha anamfanyia mume wake Brian mambo yote hayo, hata kama yeye ni mwanamke anayetengeneza pesa zake mwenyewe.
Pia anasema wanawake wamekuwa na vichwa vigumu kama wanawake wa kazi, na kuacha nyumba kuendeshwa na wafanyakazi wa ndani.
“Simruhusu shangazi ampikie mume wangu chakula, hiyo inaitwa kuwa mtiifu.”
Risper pia anasema wanawake wamekuwa walevi, wakivuta shisha kupita kiasi. Anasema hii haupati heshima ya mwanaume.