Home » Akothee: Sipendi Madharau!

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu Esther Akoth almaarufu Akothee ameibua malalamiko baada ya kujumuishwa kwenye orodha ya jarida la Forbes ya wanamuziki matajiri zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Katika taarifa yake siku ya Jumatano, mama huyo wa watoto watano alidai kuondolewa kwenye orodha hiyo akibainisha kuwa tayari amepita hatua ya kuorodheshwa miongoni mwa wanamuziki matajiri zaidi.

 

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 aliendelea kueleza kuwa kwa sasa amejikita katika kusimamia utajiri wake mkubwa.

 

“Sasa nani kaniweka kwenye orodha hii niondoe kabisa kwenye orodha hii, nilikuwa kwenye orodha ya matajiri kitambo kaka nasimamia mali yangu sipendi madharau madogo,” alisema Instagram.

 

Alibainisha kuwa ni dharau kumuorodhesha miongoni mwa wanamuziki matajiri na kutaka kujumuishwa katika orodha ya watu matajiri zaidi.

 

“Jua tofauti kati ya 1. kusawazisha bili na kusimamia mali. Ninahisi kama kuanzisha matatizo,” alisema.

 

Hivi majuzi, jarida maarufu la Forbes lilichapisha orodha ya wanamuziki matajiri zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujumuisha baadhi ya watu wenye majina makubwa katika muziki kutoka Kenya, Tanzania na Uganda.

 

Orodha hiyo ilitawaliwa sana na wanamuziki wa kiume, huku Akothee akiwa ndiye mwanamke pekee katika kumi bora.

 

Kwa mujibu wa Forbes, mwimbaji wa Uganda aliyegeuka kuwa mwanasiasa, Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine ndiye msanii tajiri zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki akiwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 9.

 

Nafasi ya pili ilichukuliwa na staa wa Bongo Diamond Platnumz ambaye utajiri wake kutokana na biashara zake za vyombo vya habari, lebo na kampuni ya ubashiri zote ni dola za Marekani milioni 8.2.

 

Mkongwe wa muziki, Jose Chameleone aliorodheshwa katika nafasi ya tatu akifuatiwa na Akothee kutoka Kenya, Profesa Jay, Alikiba wote kutoka Tanzania na kisha kufuatiwa na mwanasiasa wa Kenya Charles Njagua aka Jaguar.

 

Bosi wa Konde Music Worldwide Harmonize alitajwa katika nafasi ya nane akifuatiwa na bendi ya muda mrefu kutoka nchini Kenya, Sauti Sol.

 

Mwanamuziki wa Uganda, Bebe Cool alimaliza kumi bora.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!