Home » Satellite Ya Kwanza Ya Kihistoria Kuzinduliwa Kenya

Satellite Ya Kwanza Ya Kihistoria Kuzinduliwa Kenya

Kuanzia Wiki ijayo, mamlaka ya anga nchini Kenya yaani Kenya Space Agency, litazindua mwanga wa setilaiti yake ya kwanza katika tukio la kihistoria kupitia mpango wake wa masuala ya anga.

 

 

Satelite hiyo inayaofahamika kama Taifa 1, imepangwa kurushwa angani April 10 kwa kutumia roketi ya SpaceX falcon 9, kutokea kwenye kituo chake cha Vandenberg Space mjini Carlifonia.

 

 

Mamlaka hiyo imesema hatua hiyo ni muhimu katika maendeleo ya teknolojia kwa taifa hilo na kwamba itachangia pakubwa katika mpango wa nchi hiyo kujenga uchumi kupitia anga.

 

 

Kurushwa kwa kifaa hiki, kutaongeza nguvu ya maendeleo ya kisayansi na ubunifu kwa bara la Afrika, ambapo nchi ya Misri, ndio ilikuwa taifa la kwanza kufanya hivyo mwaka wa 1998.

 

 

Mnamo 2018, Kenya ilizindua majaribio yake ya kwanza ya satelaiti ya nano kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!