Home » Rais Ruto Awataka Majaji Afrika Kuongoza Vita Dhidi Ya Hali Mbaya Ya Hewa

Rais Ruto Awataka Majaji Afrika Kuongoza Vita Dhidi Ya Hali Mbaya Ya Hewa

Rais William Ruto ameiomba Afrika kufanya juhudi za pamoja ili kushinda vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya anga.

 

 

Ruto amesema bara Afrika limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na athari zake mbaya.

 

 

Alibainisha kuwa urekebishaji upya wa kitaasisi na uwekaji upya wa kiuchumi unaotokana na mabadiliko haya, utaiweka Afrika kama taifa lenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani.

 

 

Alikuwa akizungumza Jumatatu wakati wa Kongamano la 3 la Kikanda la majaji Barani Afrika katika Hoteli moja  Kaunti ya Nairobi.

 

 

Rais alisema changamoto inayo ambatana na hali ya  hewa yanayokuja ni ya kutisha sana kwa Afrika, hususan wakati Afrika iko kwenye kipindi cha amani na ustawi.

 

 

Aliuambia mkutano huo kuwa licha ya ukweli kwamba Afrika imejikita katika kukabiliana na umaskini na ukosefu wa usawa, njia ya uchafuzi wa mazingira sio chaguo.

 

 

Aliipongeza Idara ya Mahakama kwa kuchukua nafasi ya mbele katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.

 

 

Viongozi kadhaa walihudhuria akiwemo Naibu wake Rigathi Gachagua, Jaji Mkuu Martha Koome, majaji wakuu wastaafu David maraga na Willy Mutunga, spika wa bunge Moses Wetangula miongoni mwa viongozi wengine

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!