Home » Mwenyekiti Wa Zamani Wa IEBC Issack Hassan Achapisha Kitabu Chake

Mwenyekiti Wa Zamani Wa IEBC Issack Hassan Achapisha Kitabu Chake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Issack Hassan ametoa kitabu kipya kiitwacho “Referee of a Dirty Ugly Game” ambacho kinaelezea uzoefu wake kusimamia uchaguzi nchini Kenya.

 

Hassan alihudumu kama Mwenyekiti wa IEBC kuanzia Novemba 2011 hadi Oktoba 2016.

 

Aidha itakumbukwa kwamba Alisimamia uchaguzi mkuu wa 2013 na 2017 ambapo Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa Rais mtawalia.

 

Wakati wa uongozi wake, uchaguzi wa urais wa 2017 ulibatilishwa na Mahakama ya Juu kutokana na dosari mbalimbali zilizoshuhudiwa wakati huo.

 

Hata hivyo uchaguzi mpya ulifanyika na aliyekuwa Rais Uhuru akatangazwa mshindi.

 

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa IEBC, Hassan alihudumu kama Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Katiba ya Kenya (C.K.R.C) kuanzia 2000 hadi 2005.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!