Home » Uchunguzi Umedhihirisha Kilochomuua Mvulana Wa Miaka 12 Eldoret

Uchunguzi Umedhihirisha Kilochomuua Mvulana Wa Miaka 12 Eldoret

Uchunguzi wa mwili wa Emmanuel Kimtai aliyepatikana ameuawa, umefichua kuwa mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12 alilawitiwa kabla ya kubanwa koo hadi kufa.

 

Mwili wa mwanafunzi wa darasa la pili ulitupwa katika eneo la Koilel eneo bunge la Ainabkoi mnamo Machi 23 kaunti ya Uasin Gishu.

 

Eric Kiptoo Kipsang, mshukiwa mkuu wa kesi ya mauaji inasemekana alitupa mwili na kuelekea nyumbani kwake Kapsoya, mjini Eldoret.

 

Baadaye Kiptoo alikamatwa na maafisa wa polisi, ambapo alilalamikia maumivu ya kifua na kupelekwa hospitalini. Kisha alitangazwa kufariki Jumapili, Machi 26.

 

OCPD wa Ainabkoi Alois Muthoka, alisema Kiptoo alijaribu kujiua katika bwawa lililo karibu, na alionekana kuwa na ushawishi wa dawa za kulevya.

 

Familia ya mtoto huyo sasa imeanza mipango ya mazishi na imewaomba wahisani na serikali kuwasaidia kwani mama yake hana uwezo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!