Home » Wakenya 920 Waomba Nafasi Za Ukamishna Wa IEBC

Zaidi ya Wakenya  920 wametuma maombi ili kuhudumu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

 

Mwenyekiti wa kamati teule Dkt. Nelson Makanda, amesema wakenya mia 920 wameomba kujaza nafasi 7 kufikia mwisho wa muda wa kutuma maombi.

 

Makanda amesema kati ya waliotuma maombi  920, 25 wametuma maombi ya kushika nafasi ya mwenyekiti baada ya muhula wa Wafula Chebukati kukamilika.

 

Akihutubia wanahabari baada ya muda wa mwisho wa kutuma maombi hayo, Makanda amesema watachuja waliotuma maombi ili kujua ni nani atafuzu kwa awamu nyingine ya usaili.

 

Makanda amesisitiza kuwa licha ya mvutano wa kisiasa kuhusu jopo la uteuzi, wataendelea na majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

 

Upinzani unaoongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano mara mbili kila wiki, pamoja na masuala mengine kupinga uteuzi wa makamishna wa IEBC na jopo linaloongozwa na Makanda ambao wanadai ni wa kuegemea upande mmoja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!