Home » Haji Manara Acharuana na Mange Kimambi

 

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya soka ya Yanga Haji Manara ameingia katika mgogoro na sosholiti kutokea nchini Tanzania anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi na kuanza kujibizana kupitia mitandao ya kijamii.

 

SOMA PIA:Mabantu Kuachia University EP

 

Chanzo kimeanzia pale ambao Mange alipochapisha picha ikimuonesha mke wa tatu wa Haji Manara, Ruby akiwa na majeraha baada ya kupatiwa kipigo na Manara kutajwa kuwa ndiye aliyemfanyia ukatili huo.

 

Basi baada ya taarifa hizo kusambaa Manara akaamua kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram na kumlaani vikali Mange kutokana na tabia yake ya kuchafua watu vibaya katika mitandao ya kijamii na kuharibu hadhi zao.

 

Bila kupoteza muda naye dada Mange akajibu juu ya laana hizo kwa kueleza ya kuwa yeye naye ni Umbea ni kazi yake kama Haji manara ambavyo hutumia mdomo wake kusema maneno mabaya kwa wapinzani wake.

 

Majibu ya Mange kwa Manara

 

Pia mange ameonyesha kutokutishwa na laana hizo za Manara kwa kusema ya kuwa alishawahi kulaaniwa na hata Mashekhe wa mkoa lakini hakuna kilichomtokea na kuwa hata Haji naye ana mambo yake yasiyofaa ambayo huyafanya na kutaka ajibu ukweli juu ya chat za mkewe Ruby kama kuna uongo wowote.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!