Mabantu Kuachia University EP
Kundi la muziki kutokea Tanzania Mabantu linaliwahusisha wasanii wawili Twaa pamoja na Muuh wanatarajiwa kuachia Extended Playlist yao ya kwanza katika maisha yao ya muziki waliyoipa jina la University EP.
SOMA PIA:Harmonize Kuachia Video Ya Dakika 20
Katika ujio wa kazi yao ya kwanza kama kundi EP hiyo inatarajiwa kuwa na jumla ya ngoma nane na kwa sasa tayari wameshaachia kava ikiwa na nyimbo kama vile Muhuni, Plus 255, Serious, Kumaanisha nini, No Fia, Utotoni, Tumetoboa pamoja na Shemeji wimbo waliomshirikisha Baddest 47
Kazi hiyo inatarajiwa kuachiliwa siku ya tarehe 28 mwezi Machi majira ya saa nne asuubuhi na Mabantu wamewaomba mashabiki wao kuwapatia nafasi kwa ajili ya kusikiliza kazi yao hiyo.
Kabla ya ujio wa Universty Ep, tayari Mabantu wameshafanya kazi mbalimbali ambazo zimependwa zaidi na mashabiki wao ikiwemo Utamu, Sponsa, pamoja na Leo waliyomshirikisha Marioo.