Director Hanscana Akerwa Na Lyrics Video
Director wa video kutokea Kitanzania, Hanscana, hivi karibuni alitumia mitandao ya kijamii kuwakosoa wasanii ambao huachia video za maneno pekee (Lyrics video) bila kuambatanisha video rasmi ya muziki. Katika chapisho lake kwenye akaunti yake ya Instagram.
Hanscana alielezea kutofurahishwa kwake na ubora wa video nyingi na kuwataja wasanii ambao hivi karibuni wameachia video za maneno pekee bila kuachia video rasmi ya muziki.
SOMA PIA:Mo Jay, Gigi Money Wafikishana Polisi
Hanscana ni Director wa video anayejulikana na kuheshimiwa nchini Tanzania, baada ya kufanya kazi na baadhi ya majina makubwa katika tasnia ya muziki kama vile Diamond Platnumz, Barnaba Classic, Zuchu na wengine wengi.
Kazi yake inajulikana kwa ubora wake na umakini wa kila jambo, ndio maana maoni yake yamesababisha mjadala kati ya wasanii na mashabiki juu ya video hizo zisizokuwa na ubora. Moja kati ya wasanii ambao wamefanya jambo hilo ni pamoja na Ali Kiba katika video ya Mahaba
Katika chapisho lake, Hanscana alishiriki meme ambayo ilisema, “Hivi sasa, wasanii hutoa video za maneno pekee, na wanaamini wametimiza kitu.” Kisha aliendelea kumtaja Ali Kiba na wimbo wake “Mahaba” kama mfano wa msanii ambaye hivi karibuni aliachia video ya maneno pekee bila kuachia video rasmi ya muziki.