Home » Ali Kiba Ajiunga na Golden Club Boom Play

 

Mwanamuziki wa Tanzania, Ali Kiba, amefikia hatua mpya katika kazi yake ya muziki, baada ya kufikisha zaidi ya wasikilizaji milioni 100 kwenye jukwaa maarufu la kusikiliza muziki la Boomplay. Hatua hii inakuja baada ya kutoa wimbo wake wa “Mahaba” ambao tayari umepata zaidi ya wasikilizaji milioni 10 kwenye jukwaa hilo.

 

SOMA PIA:Esma Platnumz, Mwijaku Watia Neno Sakata La Gigy, Moj360

Ali Kiba sasa anajiunga na klabu maalum ya wasanii wa Tanzania ambao wamefikisha mafanikio haya makubwa kwenye Boomplay, akiwemo Diamond Platnumz, Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Harmonize, Marioo, na Jay Melody. Mafanikio haya ya Ali Kiba yametokana na muziki wake wa albamu na nyimbo za pekee.

 

 

Kwa mujibu wa Boomplay, Kazi ya Ali Kiba iliyosikilizwa zaidi kwenye jukwaa lao ni albamu yake ya 2021 yenye jina “Only One King“. Albamu hiyo ina nyimbo kama “Utu”, “Salute” na “Sitaki tena” ambazo zimepokelewa vizuri barani Afrika, na hivyo kumpatia Ali Kiba nafasi kubwa kama mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa Tanzania

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!