Home » KNCHR Yaitisha Uchunguzi Baada Ya Maandamano

Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) imetaka uchunguzi ufanyike mara moja kuhusu jinsi maafisa wa polisi na waandamanaji walivyoendesha maandamano ya nchi nzima jana Jumatatu ambayo yaligeuka kuwa ya machafuko.

 

Katika taarifa, mwenyekiti wa KNCHR Roseline Odede amekashifu maandamano waliyoanzisha Azimio la Umoja One-Kenya ambapo amesema yamesababisha uharibifu wa mali, majeraha na madai ya matumizi ya risasi na maafisa wa usalama.

 

Odede amebainisha kuwa wao, kwa ushirikiano na Mamlaka Huru ya Kusimamia Uchumi (IPOA), wanajitahidi kuthibitisha madai hayo na watawafikisha wahusika mahakamani wakipatikana na hatia.

 

Pia ametoa wito kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome vile vile kuangalia suala hilo, na kuhakikisha mwenendo wa polisi wakati wa maandamano unaratibiwa na kuzingatiwa.

 

Katika kauli hiyo hiyo, tume hiyo inasema waliohusika katika uporaji huo au aina yoyote ya utovu wa nidhamu wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!