Raila Asema Hasitishi Maandamano Hadi Haki Itendeke
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amesema wanataka haki ya uchaguzi itendeke na kushinikiza lazima sava ya IEBC ifunguliwe.
Akizungumza alipojumuika na wafuasi wake na kufanya mzunguko katikati mwa jiji la Nairobi, Odinga amesema leo ni mwanzo wa maandamano kwa minajili ya kutafuta usawa katika taifa hili.
” Vita imeanza na haitaisha mpaka wakenya wapate haki yao,” kasema odinga
AwaliM msafara wa Odinga ulizuiliwa kuingia katika hoteli ya kifahari ya Serena ambapo walilazimika kurusha vitoza machozi kuwatawanya watu waliokuwa wamekusanyika maeneo hayo ambayo ni kilimita chache tu na ikulu ya ya Nairobi.
Raila alikuwa ameandamana na vigogo wa Azimio wakiwemo Kalonzo Musyoka, Martha Karua na Eugene Wamalwa ambao wamelikashifu serikali kutumia polisi vibaya kuvuruga maandamano waliyotaja kuwa ya amani.
Baadhi ya wabunge wa wa upinzani wakiwemo Senator wa Kilifi Stewart Madzayo na Opiyo Wandayi wa Ugunja wamekamatwa.