Home » Mtu Mmoja Apigwa Risasi Wakati Maandamano Yakiendelea

Mtu mmoja amepigwa risasi  katika soko la Toi karibu na mtaa duni wa Kibera wakati maandamano yakiendelea kupamba moto sehemu tofauti tofauti nchini kenya.

 

Hata hivyo, inasemekana jamaa aliyepigwa Risasa  hakuwa baadhi ya waandamanaji bali alikuwa ni  fundi mitambo aliyekuwa akiendeleaza kitega uchumi yake.

 

 

Kulingana na walioshuhudia, jamaa huyo alipigwa risasi na afisa wa polisi . Hata hivyo, wakaazi walimkimbiza hospitalini kwa pikipiki mara moja.

 

Hayo yakiendelea ni kuwa Polisi wa kutuliza ghasia jijini Nairobi  wamewarusha vitoza machozi wakati wakiendelea kuwakabili waandamanaji kati kati mwa miji kafha kama vile Nairobi, Kisumu na kakamega.

 

Barabara zote za kuelekea kwenye ikulu ya Nairobi ikiwa imefungwa na njia ya kuelekea ikulu ndogo ya Kisumu pia imefungwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!