Real Madrid Kumenyana Na chelsea Katika Robo Fainali Ya UEFA

Mabingwa watetezi Real Madrid watacheza dhidi ya miamba wa uingereza Chelsea katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa bara Ulaya.
Pep Guardiola na Manchester City yake atakutana na klabu yake ya zamani Bayern Munich baada ya droo iliyofanywa leo mjini Nyon nchini uswizi.
Mabingwa watetezi wa serie A ya Italia AC Milan watashuka dimbani dhidi ya mabingwa Napoli katika mechi inayozikutanisha timu mbili za Italia.
Benfica ya ureno imeratibiwa kutoana jasho Inter Milan.
Mshindi kati ya Chelsea Na Real Madrid atakutana na mshindi kati ya Manchester city na Bayern Munich. Kisha mshidi baina ya Napoli na AC Milan apatane na mshindi kati ya Inter na Benfica.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Aprili 11 na 12 kisha mkondo wa pili utakuwa Aprili 18 na 19.