Home » Ali Kiba Akana Kushiriki Albumu Ya Davido

Ali Kiba Akana Kushiriki Albumu Ya Davido

 

Alikiba akana kuwepo kwenye Imagination Wan KILL me

Mwanamuziki na mmiliki la lebo ya Kings Music Ali Kiba, amekanusha kushiriki katika albamu ya mwanamuziki kutokea Nigeria Davido baada ya uvumi huo kusambaa.

SOMA PIA:Harmonize Aanzisha Podcast

Siku ya Jumatatu ilitoka orodha ikionesha nyimbo mbalimbali zilizotajwa kuwepo katika albamu ya Davido yenye jina la A Best Time huku king Kiba akiwa mmoja wa wasanii waliotajwa Katika orodha hiyo.

 

Katika mahojiano aliyofanyiwa, Kiba na mtangazaji Vido Vidox amethibitisha kutokuwepo na kutofahamu juu ya yeye kuhusishwa katika albumu hiyo iliyotajwa kuwa na jumla ya mikwaju 17.

 

 

Kati ya wasanii waliotajwa kuwepo katika albumu hiyo ni Ali Kiba pekee ndiye aliyetoa neno kwa kukataa kushiriki katika wimbo uliopewa jina la LET’S GO ikiwa ni track ya kumi.

 

Albumu ya Davido inatarajiwa kuachiliwa hivi karibuni baada ya kuihairisha kutokana na kifo cha mtoto wake na mkewe Chioma lakini kwa upande wa msanii huyo hajatia neno lolote juu ya ujio wa albumu hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!