Anjella Achora Tattoo Ya Harmonize

Siku ya tarehe 15 ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa msanii Harmonize na katika kusheherekea siku hiyo mwanamuziki ambaye alishawahi kuwa chini ya lebo ya Konde Gang Anjella Black Angel ameamua kuchora tattoo ya bosi wake huyo wa zamani pamoja na tarehe yake ya kuzaliwa.
SOMA PIA: Harmonize Amshukuru Mama Zuu
Katika ujumbe aliouweka katika ukurasa wake wa stori wa Instagram Anjella alionesha video fupi ikionesha baadhi ya sehemu za hatua za uchoraji wa tattoo hiyo huku akiandika ujumbe mfupi uliosema ‘ For my brother harmnize_tz Mfungua njia’
Tafsiri ya ujumbe huo inamaanisha ya kuwa Harmonize ndiye mfungua njia wa Anjella aliyomfanya afike hapo alipo kwa sasa mara baada ya Kondeboy kuona video fupi ya binti huyo katika mitandao ya kijamii na kumtafuta kwa ajili ya kuanza kufanya naye kazi.
Anjella alishawahi kuwa moja kati ya wasanii waliokuwa chini ya lebo ya Kondegang inayomilikiwa na Harmonize kabla ya lebo hiyo kutangaza kuvunja ushirikiano uliokuwepo kati ya pande hizo mbili.
Mbali na tofauti zilizopo kati ya yao lakini Black Angel hajasahau alipotoka na bado ameonesha shukurani kwa bosi wake wa kwanzanza katika kiwanda cha muziki.